Mpenzi, leo nitazungumzia mada inayohusu tabia ambayo imeshamiri katika jamii yetu ya wanawake walio kwenye ndoa na wasioolewa kupiga picha za utupu na kuzihifadhi kwenye simu zao.
Nimeamua kuzungumza na wewe suala hilo kwa sababu ni aibu kubwa kupiga picha za aina hiyo, kwanza kisheria ni kosa na wote wanaofanya hivyo wanajidhalilisha.
Hivi shoga mwenye tabia hiyo unapopiga picha hizo lengo lako linakuwa lipi maana kama mume au mchumba unaye, hivi hujui unaweza kuibiwa simu au kuipoteza halafu watu wasio na maadili wakaamua kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii?
Hebu fikiria hali watakayokuwanayo wazazi, mumeo na watoto wako mara watakapoziona picha hizo chafu ambazo kwa ufinyu wako mdogo wa mawazo uliamua kuzipiga.
Hebu fikiria hali watakayokuwanayo wazazi, mumeo na watoto wako mara watakapoziona picha hizo chafu ambazo kwa ufinyu wako mdogo wa mawazo uliamua kuzipiga.
Shoga, wengi wanaofanya kamchezo hako ka kujifotoa picha hizo lengo lao ni kuzitumia kuwanasa wanaume wakware.
Sasa inakuaje wewe mke au mchumba wa mtu unapiga picha hizo? Hiyo nia aibu na siku ambayo mtu wako atazibamba ni wazi kama ni ndoa itavunjika hali kadhalika uchumba.
Shoga yangu, kama una hiyo tabia iache mara moja kwa sababu unajidhalilisha, mheshimu mumeo kwani ni yeye pekee anayepaswa kukuona ulivyo na si mtu mwingine.

No comments:
Post a Comment