Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba ni kama hawakamatiki baada ya leo kushinda mchezo wa 10 mfululizo kwa kuifumua Mbao Fc mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro
Mabao mawili ya nahodha John Bocco na moja la Meddie Kagere yametosha kuihakikishia Simba ushindi muhimu ambao umewasogeza karibu ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 57
Azam Fc ina alama 59 hata hivyo Simba ina michezo sita mkononi hivyo ni suala la muda tu mnyama atakaa katika nafasi yake na hatimaye kutetea ubingwa waliotwaa msimu uliopita
Mabao mawili aliyofunga Bocco leo yamemfanya afikishe mabao 11 akihitaji kufunga bao moja tu kumfikia Heritier Makambo wa Yanga
Kagere amezidi kumkaribia Salim Aiyee wa Mwadui Fc mwenye mabao 16, baada ya bao lake la mkwaju wa penati alilofunga leo kumfanya afikishe mabao 14
Baada ya ushindi wa leo kikosi cha Simba kitaendelea na maandalizi ya mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe
Simba itaendelea kujifua mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa April 06 katika dimba la Taifa
No comments:
Post a Comment