Klabu ya Chelsea imetakiwa kuchukua hatua za haraka ili kumwajiri Zinedine Zidane kama Kocha wao.
Shinikizo hilo linatokana na kuwa Juventus inataka kumchukua Zidane kwa ajili ya msimu ujao wa Soka, Kuna taarifa kuwa Kocha wa sasa wa Juventus, Massimiliano Allegri anatazamiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Allegri inasemekana anataka kuachana na timu hiyo baada ya kuisaidia kutwaa taji la Serie A kwa mara ya tano mfululizo, Chelsea katika siku za karibuni inasemekana imekuwa inafanya mawasiliano na Zidane kwa ajili ya kumchukua.
Hali hiyo inatokana na mwenendo wa sasa wa kusuasua wa timu hiyo inayonolewa na Maurizio Sarri.
Juventus, hata hivyo, inasemekana inataka kumchukua Zidane, ambaye aliwahi kuchezea timu hiyo katika miaka ya nyuma, maana yake ni kuwa Chelsea inaweza kumkosa kama isipoongeza spidi ya kumnyakua.
Hata presha ya kutimuliwa kwa Sarri imepoa kidogo baada ya kusaidia Chelsea kuishinda Tottenham Hotspur 2-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu England, Jumatano iliyopita.
No comments:
Post a Comment