Baada ya hapo jana kumtimua Hans van Pluijm, uongozi wa Azam Fc unadaiwa kuwa katika mazungumzo na kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera
Kwa mujibu wa EATV, Zahera huenda akatangazwa kuwa kocha Mkuu wa timu hiyo wakati wowote baada ya makubaliano ya awali kufikiwa
Hata hivyo uongozi wa Yanga umekanusha taarifa hizo ukidai zina lengo la kuivuruga timu leo ikiwa na mchezo muhimu dhidi ya Namungo FC
Lakini huenda taarifa za Zahera kutakiwa na Azam fc zikawa na ukweli, anaweza akajiunga na timu hiyo mwishoni mwa msimu
Juzi Zahera aliweka wazi kuwa ataondoka Yanga mwishoni mwa msimu baada ya kukatishwa tamaa na hali ya kiuchumi ya timu hiyo huku akidai kukosa ushirikiano kutoka kwa wadau katika kampeni ya kuichangia Yanga
Zahera alisema amejitoa sana kuisaidia Yanga lakini wenye timu, ambao ni wanachama na mashabiki hawajitoi ipasavyo kuisaidia timu hiyo lakini wanakuwa wa kwanza kulalamika timu inapokuwa haifanyi vizuri
"Naamini kwa hiki nilichofanya hata nikiondoka Yanga hakuna mtu atalalamika kwani nimefanya kila linalowezekana kuwasaidia," alisema Zahera
Zahera alianzisha kampeni ya kuichangia Yanga ili kupata fedha za kukijenga upya kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.
Hata hivyo katika kipindi cha wiki tatu zimechangiwa Mil 21 tu, huku Mil 2 zikiwa zimetolewa na Zahera mwenyewe
No comments:
Post a Comment