Mabingwa wa kihistoria wa soka Tanzania Yanga wametinga robo fainali ya michuano ya kombe la Azam (ASFC) baada ya kuichapa Namungo Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa dimba la Majaliwa Wilayani Ruangwa
Bao pekee la ushindi lililoipeleka Yanga robo fainali liliwekwa kimiani na Heritier Makambo kwenye dakika ya 83 akiunganisha krosi murua iliyochongwa na Deus Kaseke
Ulikuwa ni mchezo wa nguvu uliokuwa na matukio mengi ya kibabe
Aidha mlinda lango Klaus Kindoki leo alikuwa katika kiwango bora akiokoa michomo kadhaa iliyoelekezwa langoni kwake
Yanga inakuwa timu ya kwanza kupata ushindi kwenye uwanja wa Majaliwa ambao ulifunguliwa mwanzoni mwa msimu huu
No comments:
Post a Comment