Leo February 1,2019 Wazazi wa msanii Nandywamefanya mahojiano na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV ambapo wamekuja kutambulisha wimbo mpya wa mtoto wao ambaye yupo nchini Kenya kwa shughuli zake za kimuziki.
Mbali na wazazi wake Nandy kukiri kuwa Ruge Mutahaba amechangia kwa asilimia kubwa mafanikio ya mtoto wao, wazazi wa msanii huyo wamesema kuwa katika ile skendo ya kuvuja kwa video clip ya mtoto wao, Ruge Mutahaba alichangia kwa asilimia kubwa kuwatuliza na kuwatia moyo katika changamoto ile iliyojitokeza.
“Nilipigiwa simu na mdogo wangu kuhusu ile video, kwa kweli ilinisikitisha sana maamuzi niliyoyaamua kipindi kile ni yeye kuacha muziki kabisa, lakini nilifikiri kuwa mtoto wangu hakuwa na tabia mbaya, ila nikasema haya ndio niliyakataa tangu mwanzo alipotuambia anataka kufanya muziki”
“Tunashukuru sana kwa zawadi ya nyumba aliyotupatia kwa kweli Nandy,amekuwa akitushirikisha sana kila akipata pesa anakuja kutuambia kuwa Mama leo nimepata million 5 au 10, yeye ni kijana angeweza kufanya kitu anachokitaka kama kununua nguo, lacewig lakini kiasi anachobaki nacho ni kidogo hadi namwonea huruma.”
“Hili ni jina la Nandelea ni la ukoo ambalo Nandy amepewa na Bibi yake Mzaa Mama yake.”, ambapo kwa mujibu wa Wazazi wake ni kuwa Bibi yake na Nandy amekuwa akifurahi sana kumuona Mjukuu wake akifanya muziki huku akiwasisitiza Wazazi wake kuendelea kumsapoti mtoto wao ili aweze kufika kimataifa zaidi”
Wazazi wa msanii Nandy wamesema ishu ya mavazi ya mtoto wao anavyovaa, kwao sio ishu, kwani ni muda wake na akiwa kama msanii ni lazima aende na trend ya muziki unavyokwenda.
No comments:
Post a Comment