We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, February 26, 2019

Watuhumiwa wa kuua kwa kukata koromeo kesi yao yasikilzwa


Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Bukoba jana imeanza kushikiliza mashahidi wa upande wa Jamhuri wa kesi ya mauaji inayowakabili watu watatu wanaotuhumiwa kuwaua kikatili kwa kuwakata makoromeo watu wanne waliokuwa wakazi wa kiijiji Chakashenge kilichoko katika kata ya Katoma iliyoko ndani ya halmashauri ya wilaya ya Bukoba , mkoani Kagera. 

Katika kesi hiyo inayowakabili Alyu Dauda Hassan, Ngesella Kea Joseph na Rashid Mzee Athumani, aliyetoa ushahidi mbele ya jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Mheshimiwa Lameck Michael Mlacha ni Inspekta wa jeshi la polisi Banda Mwita Marwa ambaye alihusika moja kwa moja wakati wa zoezi la kuwasaka na kuwakamata watuhumiwa wa vitendo hivyo vilivyokuwa vimeshika kasi mkoani humo. 

Shahidi huyo akiyeeleza mbinu zilizotumika kuwakamata watuhumiwa hao ameimbia mahakama kuwa mtuhumiwa Rashid Mzee alipokamatwa na kupekuliwa alikutwa na simu aina ya Itel iliyokuwa inamilikiwa na marehemu Kaijage John ambaye ni miongoni mwa watu wanne waliouwawa katika tukio hilo. 

Mwita aliyewasilisha simu hiyo mahakamani kama kielelezo aliendelea kuiambia mahakama kuwa simu ya marehemu Kaijage ndio ilikisadia kikosi cha upelelezi kuwapata watuhumiwa wengine wa mauaji hayo, amesema watuhumiwa wote walipoojiwa walikiri kuhusika na matukio 14 ya kuwaua kitatili kwa kuwakata makoromeo na matukio 13 ya kuchoma makanisa. Yaliyotokea Novemba 1, 2015.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list