We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, February 24, 2019

Warithi wa Kocha Mkuu wa Azam FC hawa hapa


Baada ya Azam FC kuachana rasmi na Kocha wake Mkuu  Hans Pluijm pamoja na msaidizi wake Juma Mwambusi nafasi zao zitazibwa kwa muda na makocha wa timu za Vijana.

Maamuzi hayo yamekuja kwa makubaliano ya pande zote mbili kukubaliana kutokana na kutoridhishwa na matokeo yake ya hivi karibuni ya kwenye mechi za Ligi Kuu Bara (TPL).

Kwa taarifa iliyotolewa na klabu ya Azam FC, sasa benchi la ufundi litakuwa chini ya makocha wa timu za Vijana, Meja Mstaafu Abdul Mingange (U20) na Idd Cheche (U17).

Kwa sasa Uongozi wa Azam tayari umeanza mchakato wa kumtafuta atakayerithi mikoba ya Kocha huyo raia wa Uholanzi.

Pluijm ameiongoza Azam FC kwenye michezo 25 na amepoteza michezo mitatu ameshinda 14 na kutoa sare nane akiwa na pointi 50 nafasi ya pili. 

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list