We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, February 25, 2019

Wananchi waua wanne waliosadikiwa kuwa ni majambazi

Wananchi wa kijiji cha Kinyasi wilayani Kondoa wamewaua watu wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi waliovamia kituo cha mafuta kilichopo kijijini hapo na kupora zaidi ya Sh.Milioni 10.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa adhabu ya mhalifu ni kifo.

“Hata kama wamechukua fedha nao wamepata hasara kwa kuwa adhabu ya mhalifu ni kifo, mhalifu anayekuja na panga silaha yeyote adhabu yake ni kifo tu, nguvu mliyotumia inafanana na matendo yao,”amesema.

Muroto amewataka wananchi kuwaadabisha wahalifu hadi kieleweke.

“Umoja wenu umewatisha watu wenye bunduki nawashukuru sana wananchi, nimekuja kuwashukuru na mtoe taarifa za uhalifu na uhalifu,”amesema.

Naye, Mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho, Awadh Nyundo amesema majambazi hao walifika katika kituo hicho kwa lengo la kuweka mafuta.

“Tuliwaambia tumeshafunga muda umeshaisha wakarudi kama wanaondoka lakini wakarudi mara ya pili wakanifuata ofisini wakasema niwape funguo na hesabu ya leo, zikaanza kurupushani baada ya kuwakatalia funguo, wakanibana na kufanikiwa,”amesema

Kadhalika, Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo, Dk.Frolence Hillary amesema miili hiyo ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali hiyo.

==>>Tazama hapo chini

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list