We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, February 24, 2019

Waandaaji wa SZIFF washambuliwa mitandaoni, Johari ashangazwa na washindi wa tuzo ya muigizaji bora wa kike na kiume (+video)

Jana usiku kulikuwa na ugawaji wa tuzo za filamu za SZIFF, ambapo tulishuhudia waigizaji wa filamu wa ndani wakiibuka kidedea.

Image result for SZIFF 2019

Ugawaji wa tuzo hizo, umezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii hususani kwenye kipengele cha muigizaji bora wa kike na kiume, ambapo washindi walikuwa ni Flora Kihombo na Rashid Msigala kupitia filamu yao ya KESHO.
Kiufupi hawa wote ni watoto na hata kazi yao haijapata kuonekana sana, ukilinganisha na filamu za waigizaji wengine kama Wema Sepetu, Monalisa, Gabo na wengineo waliokuwa wanashindana kwenye vipengele hivyo, jambo ambalo limezua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii.


essau_esquireMsiandae tena hizi tuzo 🤧🤧🤧 na waigizaji msiendeshwe kisa Azam ndio wanaandaa hii SZIFF. Bora ujue hujaingia kwenye mashindano kuliko kuja kuburuzwa kama mlivyofanyiwa jana

pitwhizzy@___moh.d.r.t0_lee yan ndo maana Bongo hatuendelei asee umewahi kuona wapi watoto wanapambanishwa na wakongwe kwenye category moja walishindwa kuweka category ya upcoming au… Upumbavu huo

babranlaurentNimeshangaa sana Tuzo mwigizaji bora wakike anapewa huyo dogo badara ya wema nahuyo dogo apewe Tuzo ya msanii chipukizi wa wakike nalle Tuzo ya msanii bora wa kiume kapewa dogo wa kiume anaye alitakiwa apewe Gibo dogo apewe Tuzo ya msanii bora wa kiume anaye chipukia Azam tv mmepoteza sifa kwenye hili kanumba nae mmemkaushia hata Tuzo mungu Anawaona!



qutest_48 Yani labda km Azam mna Interest Zenu binafsi ila Mmeboa mnafanya watu Wajinga! @azamtvtz

qutest_48Yani mnaenda kuyazika haya mshindano kwa mikono yenu! UPUUZI MTUPU bora ning’oe dishi la Azam nifunge Star times mxiiiiiiiu yani ni MAZINGAOMBWE Kama Tuzo za Kilimanjaro @azamtvtz

hapixlucasmnaelekea kwny nyayo za kili awards tunawazika si muda

kwa upande mwingine, Muigizaji wa Bongo Movie, Johari ambaye naye alikuwemo kwenye vipengele vya tuzo hizo amesema kuwa washindi hao wangewekwa kwenye vipengele vya wasanii chipukizi na sio kama walivyowachanganya na wasanii wakongwe.







No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list