We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, February 1, 2019

Waajiri watakiwa kuwahisha michango mifumo ya jamii

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama, ameitaka mifuko yote ya hifadhi ya jamii kuhakikisha kuwa waajiri wanafikisha michango ya wafanyakazi katika mifuko hiyo baada ya kuwakata katika mishahara yao.

Mhagama alisema hayo bungeni jana, alipokuwa akitoa jibu la nyongeza kwa Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige (CCM), ambaye alitaka kujua ni lini serikali itawalipa wafanyakazi 545 wa Kilitex-Arusha na wale wa hoteli ya Sabasaba ambao bado wanadai pensheni baada ya mwajiri wao kutowasilisha michango yao kwenye mfuko wa PPF.

Alisema bado tatizo la malipo ya pensheni kwa wafanyakazi ni tatizo kutokana na baadhi ya waajiri kutofikisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko kwa wakati.

Akizungumzia suala la wafanyakazi wa KILTEX na wa hoteli ya Sabasaba ambao wafanyakazi wake hawalipwa pensheni, Mhagama aliwataka viongozi watendaji wa mifuko inayohusika na wafanyakazi hao kukaa pamoja kutatua tatizo hilo.

Awali akijibu swali la msingi la mbunge huyo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji, alisema kwa mujibu wa kumbukumbu na nyaraka zilizoko na taratibu za ufilisi ulikamilika na wafanyakazi wa KILTEX walilipwa stahili zao.

Kijaji alisema hata hivyo, baadhi ya wafanyakazi walilipwa mafao yao ya kiinua mgongo kwa mkupuo na wengine walirejeshewa michango yao kadri walivyochangia.

Alisema utaratibu huo wa malipo ulifanyika baada ya mfilisi kushindwa kulipa riba, adhabu na malimbikizo ya michango kwenye mfuko wa pensheni wa PPF.

“Uamuzi huo ulifikiwa kutokana na ukweli kwamba, mauzo ya mali za kiwanda yalikuwa ni madogo ikilinganishwa na jumla ya madai na gharama halisi za ufilisi,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list