We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, February 23, 2019

Tarehe ya uchaguzi Yanga kutangazwa Marchi 05


Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Tanzania (TFF) imesema kuwa itatangaza hatima ya uchaguzi wa Yanga ifikapo Machi 5 mwaka huu.


Awali uchaguzi huo wa Yanga ulitarajiwa kufanyika Januari 13 mwaka huu, lakini ukaahirishwa kutokana na baadhi ya wanachama kufungua kesi mahakamani kusimamisha mchakato huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Ally Mchungahela, ameliambia gazeti la Nipashe kuwa tayari kamati yake imekutana na viongozi wa Yanga kwa ajili ya kufikia muafaka wa uchaguzi huo.

Mchungahela alisema kuwa watakachotangaza ni tarehe mpya ya kufanyika kwa uchaguzi huo lakini akaweza wazi kwamba mchakato wake hautaanza upya.

"Uchaguzi wa Yanga upo na utafanyika, Machi 5 ndio tutatangaza tarehe ya uchaguzi, wanachama wa Yanga wajiandae na uchaguzi wa klabu yao ambao utawapa viongozi wapya," alisema Mchungahela.

Aidha, alisema anaamini mpaka kufika siku hiyo kila kitu kitakuwa sawa na hakutakuwa tena na kikwazo cha kutofanyika kwa uchaguzi huo.

"Uchaguzi utaendelea pale tulipoishia, hatutaanza upya mchakato, tumekuwa na vikao vya pamoja na mara kwa mara na Yanga kwa ajili ya kuhakikisha maandalizi ya uchaguzi huu yanakamilika," alisema Mchungahela.

Aliongeza kuwa katika vikao vya pamoja walikubaliana upande wa Yanga kuwapa majina ya viongozi au wanachama watakaoshirikiana kwa karibu kukamilisha uchaguzi huo.

Uchaguzi huo uliingia katika mvutano baina ya wanachama, Yanga na TFF, jambo lililopelekea kushindwa kufanyika mpaka sasa.

Tayari uongozi wa Yanga umetangaza Kamati yake ya Uchaguzi ambayo itashirikiana na ya TFF kukamilisha mchakato huo wa uchaguzi

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list