We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, February 23, 2019

Sababu Halima Mdee kuitwa polisi hii hapa


Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee leo Jumamosi Februari 23, 2019 hadi saa 8:00 mchana alikuwa akiendelea kuhojiwa na mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kinondoni (RCO) kwa kosa la uchochezi.
Akizungumza na Mwananchi leo wakili Hekima Mwasipu amesema Mdee ameitwa polisi kwa kosa la uchochezi.
Hekima amesema kwa sasa polisi wanaendelea kumhoji kutokana na kauli alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mikocheni Februari 21, 2018.
"Polisi wamemuita kwa kosa la uchochezi kutokana na kauli alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mikocheni juzi tunaendelea kuandika maelezo,” amesema.
Mdee aliyefika kituo cha Polisi Oysterbay zilipo ofisi za RCO saa 3 asubuhi, alianza kuhojiwa  saa 6:15 mchana.
Mwenyekiti huyo wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) alieleza kuitwa kwake kituoni hapo kupitia akaunti yake ya Twitter, “Nimepokea wito kituo cha Polisi Oysterbay kwa mahojiano.”

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list