Mbunge wa Kawe kupitia (CHADEMA), Halime Mdee ameitikia wito wa Polisi Kinondoni jijini Dar es Salaam aliotakiwa kufika leo Jumamosi Februari 23,2019.
Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) ametumia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kuoleza hilo.
“Nimepata wito wa kuitwa Polisi Oysterbay kwa mahojian, mpaka sasa sababu ya wito ni nini. Ngoja tujongee.” ameeleza Halima Mdee.
Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Mbunge Joseph Mbilinyi 'Sugu' kuhojiwa na Polisi kwa saa zaidi ya tano baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Mate kumtaka Sugu kuripoti kwa ajili ya mahojiano.

No comments:
Post a Comment