Jaji Mkuu wa tuzo za Sinema Zetu SZIFF Dkt. Martin Mhando amezungumza kwa maa ya kwanza kuhusu maoni ya wadu wa filamu Tanzania, waliohoji kwanini watoto walioshinda Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume na Muigizaji Bora wa Kike walishindanishwa na waigizaji wakongwe.
Akiongea kwenye kipindi cha Morning Trumpet cha Azam TV, amesema kuwa tuzo hazikukataza watoto wasishindanishwe na wakongwe, huku akieleza kuwa muigizaji ni muigizaji haijalishi umri.
Mhando, amesema kuwa Watanzania walikuwa na washindi wao tayari ndio maana walishikwa na taharuki, huku akieleza kuwa mfumo wa utoaji tuzo ulizingatia vigezo kama zilivyo tuzo nyingine za kimataifa.
Kuhusu watoto kuwagaragaza wasanii wakongwe, Mhando amesema hilo ni jambo la kawaida kabisa na amewaasa wasanii wasitumie majina kuliko kazi.
Jumamosi ya wiki iliyopita, Tuzo za SZIFF zilitolewa ambapo watoto Rashid na Flora kupitia filamu yao ya Kesho walishinda tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume na Wakike.
No comments:
Post a Comment