We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, February 25, 2019

Haruna Moshi Boban kafunguka, DC Muro ametukosea sana

Kiungo wa club ya Yanga SC Haruna Moshi Boban baada ya mchezo wa Yanga wa Kombe la FA dhidi ya Namungo kumalizika kwa kupata ushindi wa 1-0 lililofungwa na Makambo kumalizika, alieleza masikitiko yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro baada ya kutoa kauli ambazo hawakuzipenda dhidi yake na Ngassa.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri DC Jerry Muro wiki kadhaa zilizopita alieleza na kusambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Mrisho Ngassa atafute kazi nyingine hata ukocha wa vijana maana ameisha wakati Haruna Moshi Boban akasema kuwa amechoka na maisha yake yamechoka kauli ambayo ilitafsiriwa kuwa haoni kama wanastahili kucheza Yanga.
Kufuatia kauli hiyo aliyoitoa DC Muro, Haruna amefunguka na kueleza masikitiko yake “Kweli amenidhalilisha mimi pamoja na familia yangu pamoja na club yangu, sisi wanamichezo tunakosea kuwaweka watu ambao sio wanamichezo hilo inabidi wanamichezo tuliangalie, haya ndio yanayoleta matatizo na kushindwa kuendelea kwa mpira wetu, unapoongea shirikisha kwanza Ubongo wako”
Pamoja na hayo yote baada ya siku kadhaa kupita DC Jerry Muro alitumia ukurasa wake wa instagram kuwaomba radhi wachezaji hao pamoja na club, kama utakuwa unakumbuka vizuri Jerry Muro aliwahi kuwa afisa habari wa club ya Yanga kabla ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list