Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni linaendelea kumshikilia mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi katika mkutano wa hadhara alioufanya Mikocheni Februari 21, 2019.
Mdee ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) alikamatwa jana Jumamosi Februari 23, 2019 na kunyimwa dhamana.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Februari 24, 2019, Hekima Mwasipu ambaye ni wakili wa Mdee, amesema, “Bado tunaendelea kufuatilia dhamana yake maana jana baada ya mahojiano walimuweka mahabusu na kumnyima dhamana. Leo tunaendelea kufuatilia kama kutakuwa na uwezekano wa kupata dhamana.”
Mdee anadaiwa kusema, “mtu ananunua ndege badala ya vifaa vya zahanati hii ni akili au matope.”

No comments:
Post a Comment