Habari njema kwa wanaSimba hii hapa
WAKATI Simba wakiwa wanajiandaa na mchezo kati ya Lipuli Fc utakaofanyika Jumanne 26 February 2019 akili zao pia zinawaza mchezo wa kimataifa wa Js Saoura Ugenini.
WAKATI combination ya Wawa na Juuko ikionekana kuunga Lakini tambua kuwa Juuko atakosekana kwenye mchezo unaofuata wa kimataifa kutokana na kuwa na kadi nyingi za njano zinazomzuia kucheza mchezo unaofuata.
Sasa habari njema ikufikie msomaji wa Kwata unit kuwa Beki kisiki Erasto Nyoni tayari yuko fiti na huenda akacheza hata katika mchezo wa Jumanne dhidi ya Lipuli Fc na kisha 9 March akacheza mchezo dhidi ya Js Saoura nchini Algeria.
“Kusema kweli kwa sasa nipo fiti, madaktari wamenithibitishia hivyo, bila shaka naamini endapo hakutatokea chochote basi nitakuwa tayari kuwa sehemu ya michezo yetu ijayo na hata ule wa marudiano dhidi ya JS Saoura nchini Algeria.
“Kikubwa naendelea kumuomba Mungu anipe uzima zaidi kwani tangu nimeanza mazoezi kila mmoja anaridhishwa na mwenendo wangu hii ni kwa wachezaji wenzangu, makocha na daktari kwa ujumla wao tayari wameshanipa baraka zao,” alisema Nyoni.

No comments:
Post a Comment