Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama wataendelea kuwa karibu na Wananchi pamoja na kwenda kuwasikiliza changamoto zinazowakabili, itawafanya Wananchi waendelee kukiunga mkono Chama hicho na kuendeleza ushindi katika Uchaguzi mkuu wa 2020.
Hayo yamesemwa na Rais wa Zanzibar wakati akizungumza na Viongozi wa CCM wa Wilaya ya Wete Pemba, amewataka viongozi wa majimbo wakiwamo wawakilishi na wabunge kwenda kwa wananchi wao ili wajue changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi sambamba na kuwa nao karibu ili kukiimarisha Chama hicho.
Pia amesema CCM haitamridhia Kiongozi wa Jimbo ambaye amechaguliwa na Wananchi, lakini amekuwa haonekani Jimboni na kusahau wajibu wake wa kwenda kuwatumikia Wananchi.
Makamu Mwenyekiti huyo alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na CCM, itaendelea kutekeleza majukumu yake ya kuwapelekea maendeleo endelevu wananchi wote wa Unguja na Pemba bila ya ubaguzi.
Alieleza kuwa CCM itahakikisha wananchi wote wanapata huduma sawa na bila upendeleo kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni.
Dk. Shein aliwataka Viongozi wa CCM na Serikali kufanya ziara za kuwatembelea wananchi ili kujua matatizo waliyonayo na kuyatafutia ufumbuzi badala ya kukaa ofisini.

No comments:
Post a Comment