Klabu ya Azam Fc imetangaza kusitisha mikataba ya kocha Mkuu wa timu hiyo Hans van Pluijm na Msaidizi wake Juma Mwambusi
Uongozi wa Azam Fc umechukua hatua hiyo kufuatia mwenendo usioridhisha wa timu hiyo kwenye ligi
Azam Fc imecheza michezo mitano mfululizo bila ya kushinda jana ikifungwa mabao 3-1 na Simba
Pluijm alitua Azam Fc mwanzoni mwa msimu akijiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Singida United ambayo aliitumikia kwa msimu mmoja
Pluijm amewahi kuiongoza Yanga kwa mafanikio, akishinda taji la ligi kuu misimu ya 2014/15 na 2015/16
No comments:
Post a Comment