Yanga wataja wachezaji watakaokosekana dhidi ya Biashara kesho
Kesho 31 January 2019 kikosi cha Yanga kitashuka dimbani kucheza dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup.
Kuelekea mchezo huo Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa Yanga itawakosa wachezaji wawili kuelekea mchezo huo ambao ni Jaffary Mohammed na Baruan Akilimali.
“Wachezaji wetu wote wapo na morali ya kupambana, ila wachezaji wetu wawili ambao ni Jafary Mohamed na Baruan Akilimali wataokosa mchezo wa kesho.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao tunawaheshimu wapinzani wetu na tunajua utakuwa ni ugumu ila hesabu zetu ni kupata matokeo,” alisema Saleh.
No comments:
Post a Comment