Leo Alhamisi Januari 31 2019 saa moja jioni, vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga watashuka katika dimba la Taifa kuikabili Biashara United katika mchezo wa raundi ya nne ya michuano ya kombe la FA (ASFC)
Hii itakuwa mara ya pili msimu huu kwa Yanga kuikabili Biashara United katika dimba la Taifa timu hizo zikikutana kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa ligi na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyowekwa kambani na beki Abdallah Shaibu na Heritier Makambo
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani leo ili kuwapa sapoti mabingwa hao wa kihistoria ili waweze kupata matokeo mazuri na kutinga raundi ya tano ya michuano hiyo
Viingilio vya mchezo huo ni Tsh 10,000/- kwa majukwaa na VIPna Tsh 3,000/- Mzunguuko
Baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo, Yanga imepania kurejesha tabia ya ushindi katika mchezo huo ambao mshindi wake atapambana na Namungo Fc kwenye mchezo wa raundi ya tano
Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kikosi chake kamili baada ya wachezaji wake wengi waliokuwa majeruhi kupona na kurejea kikosini
Winga Baruani Akilimali ndio mchezaji pekee ambaye ni majeruhi katika kikosi cha Yanga
No comments:
Post a Comment