We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, January 30, 2019

Taarifa kutoka Ikulu Rais Magufuli ameteua Wakurugenzi wawili na Wenyeviti wawili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Islam Seif Salum Mchenga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority – DSFA).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Mchenga umeanza December 1, 2018 na kwamba kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Zanzibar.
Wakati huo huoRais Magufuli amemteua Dkt. Emmanuel Andrew Sweke kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).
Uteuzi wa Dkt. Sweke umeanza December 1, 2018 na kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Utafiti wa Uvuvi Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tanzania Livestock Research Institute – TAFIRI) – Kigoma.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Sebastian W. Chenyambugakuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI).
Uteuzi wa Prof. Chenyambuga umeanza tarehe 26 Januari, 2019.
Halikadhalika, Rais Magufuli amemteua Prof. Justinian Rwezaula Ikingura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania – GST)

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list