Kiungo wa kati wa klabu ya Manchester United Mbelgiji Marouane Fellaini ameridhia makubaliano binafsi mkataba wa kibinasi na klabu ya Shandong Luneng kwa lengo la kuhamia klabu hiyo ya China.
United wamekataa kutoa tamko lolote ikiwa malipo yoyote yamefikiwa kumnunua mchezaji huyo raia wa Ubelgiji ambaye alitia saini nao mwaka 2018.
Katika Press iliyofanyika baada ya mchezo wa jana usiku Kocha wa muda wa Manchester United Ole Gunnar alipoulizwa na mtangazaji mmoja kuwa “Kuna tetesi zozote zinazomhusu Fellain za kuongeza mkataba….?
Ole alijibu ” Hapana sijui maana nimekuwa bize sana siku hizi kwahiyo sijui chochote kinachoendelea kuhusu yeye, ni vyema kukaa na kusubiria kipi kitatokea”
Fellaini, 31, alikuwa mchezaji mkubwa wa kwanza aliyesainiwa baada ya enzi ya Sir Alex Ferguson, akijiunga na Manchester Utd kwa kima cha pauni milioni 27.5 mwaka 2013 akitokea Everton.
Mwisho wa dirisha la uhamisho wa wachezaji katika ligi ya China ni Februari 28.
Fellaini alitia saini kandarasi mpya ya miaka miwili Old Trafford mwezi Juni mwaka jana lakini hajawahi kukubalika na mashabiki wa United licha ya kukonga nyo za mameneja David Moyes, Louis van Gaal na Jose Mourinho.
No comments:
Post a Comment