We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, February 1, 2019

SIMU YA ZITTO KABWE YASHIKILIWA NA TAKUKURU

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeishikilia simu ya mkononi ya Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwekwa ajili ya uchunguzi kuhusu tuhuma zake kwa baadhi ya viongozi wa Serikali aliyodai wamehongwa ili kukwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na mke wa Mbunge huyo kupitia Twitter, imesema TAKUKURU imeishikilia simu hiyo kwa ajili ya uchunguzi huku akiwataka ndugu, jamaa na marafiki kutoitumia simu hiyo (kuipigia au kuiandikia ujumbe) kwa sababu kwa sasa haipo mikononi mwa Zitto.
Mwishoni mwa maka jana, Zitto alilalamika kupitia mitandao ya kijamii hususan Twitter akisema mradi wa Mchuchuma na Liganga unahujumiwa na makampuni ya chuma kutoka China, Urusi na Uturuki na kudai wapo baadhi ya viongozi wa juu Serikalini katika mradi wa uzalishaji chuma wa Mchuchuma na Liganga, ambapo aliitwa TAKUKURU na kupeleka ushahidi wake.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list