BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetoa ratiba mpya ya michezo ya Ligi Kuu ili kumaliza viporo vyote kabla ya Aprili.
Hatua hiyo imekuja siku chache kufuatia wadau wa soka kuilalamikia bodi hiyo kushindwa kupanga ratiba nzuri hali inayosababisha baadhi ya timu ikiwemo Simba kuwa na viporo vingi ambavyo vinaweza kuchangia kupoteza ushindani.
Ratiba hiyo inaonesha, Simba inayoshiriki michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya mechi yake dhidi ya Al Ahly itacheza mechi zake za viporo kila baada ya siku tatu.
Akizungumza jana Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Boniface Wambura alisema wameshatoa ratiba ya mechi za viporo vitakavyochezwa kwa timu ya Simba ,Mtibwa Sugar,Yanga na Azam FC.
Nia yetu ya kupanga ratiba hii mpya ni kuhakikisha tunapoenda kwenye raundi tano za mwisho timu zote ziwe zinafanana kwenye michezo, tunajua Simba watakuwa na mechi nyingi watakuwa wanacheza kila baada ya siku tatu tumefanya hivyo ili kuondoa viporo vyote
No comments:
Post a Comment