Mshambuliaji Sadney Urikhob aliyekuja kwa majaribio katika timu ya Simba SC amerejea kwao nchini Namibia.
Mshambuliaji huyo alikuja nchini kufanya majaribio hayo huku kocha Patrick Aussems akiwa ameonyesha kuridhishwa na kiwango chake.
Taarifa imesema Kocha Aussems ameahidi kushughulikia suala lake baada ya mechi dhidi ya Al Ahly huku Hunlede Kisimbo amefeli majaribio.
Straika huyo alicheza mechi 2 za michuano ya Sportpesa Cup, Taarifa za chini ya kapeti zinasema Kocha Aussems kishafanikisha juu ya usajili wake anaweza akasaini mkataba wa mwaka mmoja au miwili.
No comments:
Post a Comment