Kipa Biashara : Nilikuja Tanzania kucheza Yanga
Kipa wa Biashara United ya mkoani Mara Nurdin Barola amefunguka mengi baada ya mchezo kati ya Yanga na Biashara United kumalizika kwa Yanga kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
Kipa huyo alionekana kuchukizwa baada ya kufanyiwa mabadiliko mwishoni mwa mchezo huo baada ya biashara kufungwa bao la pili na matokeo kuwa sare ya bao 2 kwa 2.
Baada ya kutoka alionekana akimlaumu waziwazi kocha Amri Said kiasi cha kuonekana kurushiana maneno mpaka akatolewa nje ya uwanja na makamishna wa mchezo huo.
Sababu za Kugombana na Kocha wake.
Kipa huyo ameeleza kuwa hakuona sababu ya yeye kutolewa katika mchezo huo kwani alikuwa bado anataka kuitumikia timu yake na alikuwa amedhamiria kuhakikisha wanashinda katika mchezo uo.
Akielezea kuhusu magoli Barola alisema goli la kwanza ilikuwa ni penati ambayo kudaka ni bahati nasibu lakini bao la pili yalikuwa ni makosa ya mlinzi wa Biashara ambaye alichanganyana na kipa
Nurdin Barola : Nilikuja Tanzania kucheza Yanga.
Akizungumza baada ya mchezo huo kipa wa Biashara United alifunguka kuwa alikuja Tanzania kwaajili ya kucheza Yanga na alivyotua Tanzania akitokea Burkinafaso alikuwa amealikwa na watu wa Yanga lakini alipofika Airport hakuna aliyekuja kumpokea.
Baada ya kukaa Tanzania katika jiji la Arusha visa yake ya kukaa Tanzania ilikuwa si ya muda mrefu na Yanga hawakuonekana kuwa na shida naye aliamua kwenda kuisaidia Biashara United huku ndoto zake zikiwa ni kucheza klabu kubwa kama Yanga na aliamini ipo siku ataweza kufanikisha.
Nurdin aliendelea kusema kuwa hata sasa Yanga wakisema wanamuhitaji yeye yuko tayari kwani mkataba alioingia na Biashara haukumfunga kufanya Hivyo lakini pia hata kama siyo Yanga mipango ni kucheza timu kubwa kwani anaamini anauwezo mkubwa.
Naondoka Kurudi Burkinafaso.
Kipa huyo ameeleza kuwa kwasasa akirejea mkoani Mara ataenda kuchukua kilichochake na kurejea kwao Burkinafaso kwani haoni sababu ya kuendelea kucheza Biashara United kwani kocha wake alionekana kutoenda naye sawa toka siku anaingia klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment