Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kama wachezaji wake wangekuwa makini, mchezo wa leo dhidi ya Biashara United usingefika kwenye changamoto ya mikwaju ya penati
Aidha Zahera amemshukia mshambuliaji wa tmu hiyo Mcongomani Heritier Makambo kuwa kiwango chake kimeshuka sana
Katika michezo ya hivi karibuni Makambo amekuwa akikosa nafasi nyingi za kupachika mabao
Zahera amesema Makambo tangu arudi kutoka mapumziko kwao Congo, kiwango chake kiko chini
"Huyu sio Makambo ninayemfahamu mimi, kiwango chake kimeshuka sana" amesema Zahera
"Kwani kama angekuwa kwenye ubora wake, naamini mchezo wa leo usingefika hatua ya penati"
Yanga ililazimika kupata ushindi kupitia mikwaju ya penati baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Biashara United
No comments:
Post a Comment