Nyota wa klabu ya Barcelona, na timu ya taifa ya Brazil Philippe Coutinho amejikuta akimmwagia sifa na kumshukuru Nahodha wa timu hiyo ya FC Barcelona Lionel Messi katika mchezo wa jana usiku dhidi ya Sevilla baada ya kumuachia penati.
Ikumbukwe kwamba Messi ndio mpiga penati wa klabu hiyo lakini katika mchezo muhimu wa kuhitaji matokea katika kombe la Copa del rey Messi aliona isiwe tabu ngoja nimuachie na Coutinho acheze penati leo.
Penati hiyo ndio lilikuwa bao la kuongoza na hadi mwisho wa mchezo Barcelona walishinda goli 6-1.
Coutinho aliongea na maneno haya kuhusu Messi wakati anaizungumzia penati yake:-
“Kwanza nitoe shukrani zangu kwa Lionel Messi, kwa kuniruhusu niupige mkwaju wa Penati, hiyo ni nzuri sana kwa kujengeana imani tukiwa kama timu”.
“Tulijua kwamba ili tuweze kushinda, tulipaswa kujenga ushirikiano kutoka mwanzo wa mchezo.”
“Mkwaju ulikuwa wa kawaida sana na kitu alichokifanya Messi kinaonesha jinsi ukubwa wake ulivyo”
Mpaka sasa katika michuano hiyo ya Copa del Rey Barcelona wameungana na Real Betis,Valencia na mmoja ya timu kati ya Real Madrid au Girona ambazo zitacheza usiku wa leo alhamisi.
No comments:
Post a Comment