We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, October 14, 2019

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi.

Leo tumekuletea habari njema ni kuwa tayari App mpya ipo playstore na unaweza kuidownload hapa chini ili kuendelea kupata habari zetu.

BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD APP YETU MPYA UKISHA BOFYA BONYEZA NENO OPEN IN PLAYSTORE KISHA INSTALL APP YETU MPYA!! NI RAHISI TU

Wednesday, October 2, 2019

Duniani Leo October 2, 2019 ( Sauti ya America VOA )

Bonyeza play hapa chini kutazama zaidi pia tembelea app hii kila Mara kusoma Habari Mpya

Mbunge CCM awajibu wanaosema hali ni ngumu

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Abdallah Mtolea, amewatia moyo wale wote wanaolalamika kuhusu hali ngumu, kwakuwa ugumu wa maisha ndiyo kipimo cha maendeleo kwa mtu na kwamba hakuna nchi yoyote ambayo ilishawahi kuendelea bila kupitia nyakati ngumu

Mbunge Mtolea ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio, ambapo amekiri kuwa hali ni ngumu na kuwataka wananchi wawe wavumilivu.
"Wengi wanasema hali ni ngumu ila niwaambie, hakuna nchi ambayo iliendelea kwenye hali ambayo ni nyepesi, lazima tupate maendeleo kwenye hali ngumu." amesema Mtolea.
Aidha akizungumzia suala la kuhama chama, Mtolea amesema kuwa hana mpango huo na ataendelea kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
''2020 nitaendelea kuwa Chama Cha Mapinduzi, uzuri ukiwa CCM ukienda kwa kiongozi wa Serikali unakuwa kama umeenda kwa Baba, yaani ndiyo maana kila kitu kinaenda kiurahisi'' amesema Mtolea.

"Tunarudi kileleni tunakostahili" - Nugaz

Kuelekea mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kati ya Yanga na Polisi Tanzania, Msemaji na Afisa Muhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz amesema kuwa sasa wamerejea rasmi katika ligi na watatembeza kichapo kwa yeyote atakayetokea.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital katika Makao Makuu ya Klabu hiyo, Nugaz amesema kuwa kesho Alhamisi, mashabiki wa Yanga wantakiwa kuja kufurahi uwanjani kwakuwa kazi waliyonayo hivi sasa ni kukusanya kila pointi tatu zilizo mbele yao.
"Polisi Tanzania tulishawahi kucheza nao mechi ya kirafiki na tukapoteza dhidi yao, lakini wajue kabisa unapokuwa na Yanga mashindanoni ni tofauti kabisa unapocheza nayo kirafiki, hilo walizingatie", amesema Nugaz.
"Tunataka mashabiki wetu wafike uwanjani kusapoti timu yao, kesho tumejipanga kupambana kuhakikisha kila anayeshuka Dar es Salaam na hata nje ya Dar es Salaam tunachukua pointi tatu kuhakikisha tunarudi kileleni ambako Yanga inastahili kukaa", ameongeza.
Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 na sasa iko katika nafasi za mwisho za ligi, ikiwa imecheza mchezo mmoja pekee.

Yaelezwa Pundamilia wa ajabu, aliyepatikana Kenya amehamia Tanzania, Fahamu zaidi

Pundamilia wa ajabu ambaye hivi karibuni alionekana katika mbuga ya wanyama ya Mara nchini Kenya amevuka mpaka na kuingia ndani ya Mbuga ya Wanyama ya Taifa ya Serengeti pamoja na pundamilia wengine waliokuwa wanahama pamoja na Nyumbu , limeripoti gazeti la Nation nchini Kenya
Kinyume na pundamilia wengine wenye mistari kwenye ngozi yake pundamilia huyo anamadoadoa meupe na mistari michache myeupe inayofifia mwilini mwake, jambo lililomfanya kuwa ni wa kipekee.
Taarifa ya kuhamia kwake nchini Tanzania imethibitishwa na makumi ya watalii na walinzi wa mbuga za wanyama pamoja na katibu wa shirika la madereva wa magari ya utalii nchini Kenya Felix Migoya ambaye amesema kuwa punzamilia huyo mchanga mwenye umri wa mwezi mmoja hivi , kwa sasa yuko katika eneo la kaskazini mwa mbuga ya wanyama ya Serengeti Serengeti.
Alipinga taarifa za uvumi kwamba kivutio hicho kipya cha utalii katika mbuga ya wanyama ya Mara kilikamatwa na kufungiwa kuhifadhiwa mahali pake kama ilivyoelezwa katika mitandao ya habari ya kijamii katika kipindi cha wiki tatu zilizopota, Limeripoti gazeti la Daily Nation nchini humo.
“Taarifa za mitandao ya kijamii ni feki , pundamilia anayeonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii ni mkubwa na alikamatwa nchini Afrika Kusini katika tarehe ambayo haijulikani mika kadhaa iliyopita ,”alisema Bwana Migoya alipozungumza na gazeti la the Nation Jumatano.
Wazazi wa pundamilia huyo mchanga wako katika kipindi cha mwaka cha kuhama kwa zaidi ya mamilioni ya wildebeest baina ya mbuga ya wanyama ya Serengeti na hifadhi ya wanyama ya Maasai Mara – tukio ambalo huwavutia watalii kutoka maeneo mbali mbali duniani.

PundamiliaHaki miliki ya pichaNATION MEDIA GROUP

Tukio hilo, ambalo liliwekwa katika orodha ya ”Maajabu Saba ya Dunia ‘, kwa kawaida kuanza katikati ya mwezi Juni hadi mwezi Oktoba.
Katika kipindi hiki, nyumbu hukutana kabla ya kufanya safari yao ya kurejea sambamba na mamia ya pundamilia , swala na wanyama wengine wanaotafuta malisho.
Pundamilia huyu wa ajabu mweusi kwa mara ya kwanza aligunduliwa na kupigwa picha mapema mwezi Septemba karibu na mto Mara River na Antony Tira, mwongozaji maarufu wa safari za watalii kutoka kabila la Maasai na alimpiga picha hiyo katika kambi ya utalii ya Matira Bush iliyopo ndani ya mbuga ya wanyama.
Bwana Tira alimuita pundamilia huyo mchanga jina la baba yake ‘Tira’.
Si mweusi kabisa , na kutokana na utofauti wa ngozi yake katika sehemu mbali mbali za mwili wake: “Kutokana na rangi yake , pundamilia huyo amekuwa maarufu ghafla na amekuwa kivutio cha watalii katika mbuga ya Mara na sasa huenda watalii wakaelekea Serengeti kwani watu wengi wanamfuata kiumbe huyo wa ajabu ,” aliongeza Bwana Migoya.
Tangu mpigapicha Tira alipotuma picha ya pundamilia huyo na kuwaalika watu kuja kumuona, watu wengi wamekuwa wakiongezeka katika hifadhi ya wanyama ya Mara na kusababisha ‘msongamano ‘ mkubwa wa watukatika hifadhi hiyo..

RUKWA: Wapigwa na radi wakinywa pombe kilabuni, Wanne wafariki dunia papo hapo

Watu wanne wamekufa papo hapo na wengine 7 kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi wakiwa kilabuni wakinywa pombe katika kitongoji cha Nkata kijiji cha Kate, Nkasi mkoani Rukwa.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kate, Amesema kuwa watu hao walikuwa wanakunywa pombe katika kilabu hicho, ghafla ilipiga radi katika eneo hilo,  hali iliyosababisha watu wengi kuanguka na kupoteza fahamu.
Baada ya kuwafanyia uchunguzi watu hao waliokuwa katika kilabu hicho, Mwenyekiti amesema  ilibainika wanne kati yao wamefariki dunia papo hapo na wengine kujeruhiwa na kupelekwa kwenye zahanati ya Kanisa Katoliki iliyoko kijijini hapo. Ambapo baada ya kufikisha hapo kwa huduma, wengine walizinduka na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Mwenyekiti huyo aliwataja waliofariki dunia kuwa ni John Sumuni (31), Akleo Feluzi (45), Boniface Fundililwa (38) na Anastazia Njali (48) wote wakazi wa kijiji hicho.
Naye, Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Kate Mission, Elly Joseph, alikiri kuwapokea majeruhi zaidi ya 10 na baada ya kuwapatia huduma ya kwanza, wengi wao waliruhusiwa kurudi nyumbani na wanne waliokuwa  mahututi walibaki na wanaendelea na matibabu.
Tayari Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuthibitisha kuwa watu wanne ndio waliopoteza maisha na kuwa wako kwenye kikao baada ya hapo yeye na viongozi wenzake watakwenda katika kijiji hicho kuwajulia hali majeruhi na kushiriki mazishi ya watu waliopoteza maisha.
Chanzo: Nipashe

Mahakama Kuu Kanda Ya Dar Es Salaam Kusikiliza Kesi 3,372

Na Aziza Muhali- (SJMC)
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, inaendelea kusikiliza kesi 3,372 zilizosajiliwa Mahakamani hapo kwa sasa, zikiwamo za madai, jinai na ardhi.

Hayo yamesemwa na Naibu Msajili Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Joachim Tiganga, wakati akitoa elimu kwa umma kuhusu utoaji wa huduma  zinazotolewa  na mahakama hiyo, uliofanyika leo, Oktoba 2, mwaka huu katika ukumbi wa Mahakama Kuu, uliopo jijini Dar es Salaam.

Mhe. Tiganga  alisema  lengo la kutoa elimu hiyo  kwa wananchi ni kueleza huduma zinazotolewa na mahakama hiyo pia kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wateja wao.

Akifafanua kuhusu kesi hizo, alisema kesi zinazoripotiwa kwa wingi ni kesi za madai ya kawaida ambazo ni 2,169 zikifuatiwa na kesi za jinai 789, wakati kesi za ardhi ni 354.

“Hivyo kutokana na idadi hiyo ya kesi, jaji mmoja anasikiliza kesi zipatazo 450 kwa mwaka badala ya kesi 220 kutokana na kuwepo kwa idadi ndogo ya majaji” alisema.

Aliongeza kuwa Mahakama hiyo ina jumla ya majaji saba, wakati idadi kamili inayohitajika ni 15, hivyo ina upungufu wa majaji 8.

Akizungumzia kuhusu ukataji rufaa, ambapo baadhi ya wananchi walitaka kufahamu juu ya utaratibu wake,ambao ni Farida Mwalwaka mkazi wa Toangoma na Ally Idd mkazi  wa Majimatitu, jijini Dar es Salaam, alisema kwamba mahakama  huwawezesha wateja wake kukata rufaa kwa kuwapatia nakala za kumbukumbu zote za kesi.

Aidha  Tiganga  aliwataka wananchi wenye malalamiko kuhusu uendeshwaji wa kesi mbalimbali  kufika katika dawati la malalamiko ambalo hufanyika siku ya Jumanne na Alhamisi kila wiki.

Kwa upande wake Hakimu Mhe. Joyce Karata, amewataka wananchi kuwa makini wakati wa utaratibu wa ukataji wa rufaa ambapo amesema kuwa rufaa inatakiwa kukatwa ndani ya muda, ili kuondoa usumbufu wa upatikanaji wa nyaraka.
Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list