Mshambuliaji Wilker Da Silva amepona majeraha na yuko tayari kuanza kuitumikia Simba michezo ijayo
Wilker ni mmoja wa wachezaji watatu waliosajiliwa kutoka Brazil. Hata hivyo bado mashabiki wa Simba hawajamuona ndani ya uzi wa mabingwa hao wa Tanzania Barakutokana na kusumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu
Mkali huyo wa kuzifumania nyavu, ameanza mazoezi na wachezaji wengine jana na pengine huenda kocha Patrick Aussems anaweza kumtumia kwenye mchezo wa ligi utakaofuata ambao ni ugenini dhidi ya Kagera Sugar

No comments:
Post a Comment