Taarifa iliyotumwa kwa umma na ofisi ya wizara hiyo imeeleza, Lugola amesema hayo leo Jumapili Septemba 1, 2019 wakati alipokuwa anakagua vituo vya bodaboda na bajaj, Moshi mkoani Kilimanjaro alipokuwa akikagua vituo vinavyotumika kuegesha bobaboda na bajaji.
Lugola amesema ushirikiano kati ya viongozi au askari waliopo chini ya halmashauri nchini ipo ndani ya sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi Sura namba 322, hivyo Jeshi lake linapaswa kushirikiana na Polisi Wasaidizi waliopo chini ya halmashauri ya Miji, Wilaya, Manispaa na Jiji kwa mujibu wa sheria.
Agosti 2019, Lugola alifanya mkutano na wamiliki na waendesha bodaboda na bajaj mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kutatua migogoro mbalimbali waliokuwa wanailalamikia Manispaa ya Moshi kuwanyanyasa pamoja na kuwafukuza kuegesha kituo cha Sharif una Aghakan mjini humo ambapo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabara mkoani humo aliwaelekeza wawepo katika eneo hilo.
“Askari wa usalama barabarani, muache visingizio kuwa ukamataji wa bodaboda ni mgumu hasa mnapowaandikia makosa walipe baada ya siku saba, mara husingizia bodaboda hazipo katika mfumo wa (Mamlaka ya Mapato Tanzania) TRA kama magari.”
“Tukiziachia tuzipate wapi, nilishawaelekeza mshirikiane na viongozi wa serikali za mitaa, vijijini, miji, manispaa na jiji kuanzisha kanzi data, kwenye mfumo wa kuwasajili waendesha bodaboda wote sehemu mbalimbali nchini na taarifa za bodaboda hizo endapo zinafanya makosa inakua rahisi kuzikamata kwa sababu zipo kwenye mfumo,” amesema Lugola.
Amesema lengo la usajili wa bodaboda huo ni kutokana na kuepuka kuzikamata hovyo na kuziweka vituoni jambo ambalo analipinga kuepusha mlundikano wa boaboda vituoni na pia kuwasababishia bodaboda hao kuwaongezea umaskini zaidi.
“Naomba niendelee kurudia tena agizo hili, bodaboda zinazopaswa kuwepo vituo vya polisi ni za aina tatu, moja bodaboda zilizotumika katika matukio ya uhalifu, mbili zilizohusika katika ajali na tatu, bodaboda zilizookotwa, mbali na makundi hayo zinapaswa kulipwa faini,” amesema Lugola.
Pia Lugola amewataka baadhi askari na wananchi kuacha tabia ya kuwatuhumu viongozi wanapowatetea waendesha bodaboda wanaambiwa wanasiasa ndiyo wanasababisha ajali kuongezeka.
Amesema kauli hiyo sio sahihi, kwani wanaosababisha ajali asilimia 76 kwa mujibu wa utafiti wa ajali zinazotokea barabarani zinasababishwa na makosa ya wanadamu na sio bajaj na bodaboda peke yao na asilimia 24 za ajali zinatokea zinasababishwa na ubovu wa miundombinu.
“Kumekuwa na dhana potofu kwamba wanasiasa kama mimi tunasababisha ajali za bodaboda, kwa sababu tunawatumia bodaboda kwa mgongo wa siasa, sasa nataka niwaambie, wanaosababisha ajali barabarani ni asilimia 76 ni makosa ya wanadamu ambao ni wanadamu watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, wenye mikokoteni, wanafuga mifugo barabarani na madereva ndio wanasababisha ajali na sio bodaboda wala bajaj peke yao,” amesema Lugola.
Lugola amesema hakuna mahali popote ambayo tumesema baodaboda wakifanya makosa wasikamatwe, tunachosema na kusimamia ni kupunguza umaskini kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo inaelekeza bodaboda na bajaj wafanye biashara ili wapunguze umaskini.
No comments:
Post a Comment