Beki kisiki wa Yanga Vicent Andrew Chikupe huenda akajiunga na timu hiyo jijini Dar es salaam baada ya kufikiwa makubaliano kuhusu suala lake
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema viongozi wa timu hiyo pamoja na yeye mwenyewe wamefanya jitihada kuhakikisha Dante anajiunga wenzake kuendelea na majukumu
"Tumesimulia na Dante, mambo yake yanamalizwa na viongozi nafikiri atajiunga nasi siku yoyote," amesema
Yanga inatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam kesho Jumatano, kumalizia maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO United
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa Jumamosi, Septemba 14 2019

No comments:
Post a Comment