Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa pole kwa familia ya Christopha Rupia, shabiki aliyepoteza maisha kwenye mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Burundi uliopigwa uwanja wa Taifa Jumapili, Septemba 08
Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred leo alifika nyumbani kwa marehemu nje kidogo ya jiji la Dar es salaam kuwasilisha salamu pamoja na rambirambi
Mzee Rupia alipoteza fahamu uwanjani baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo kisha kukimbizwa Hospitalini ambako alipoteza maisha
Alikuwa ni shabiki mkubwa wa timu ya Taifa na inaelezwa siku ya mchezo ni kosakosa za mabao ndizo zilizomfanya akumbwe na shambulizi la moyo
Mzee Rupia anatarajiwa kuzikwa Jumamosi
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema, peponi AMEN.

No comments:
Post a Comment