We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, September 13, 2019

TFF imefafanua madai ya Amunike

Shirikisho la Soka nchini (TFF) limesema halijapokea taarifa yoyote kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) juu ya madai ya kocha wa zamani wa Taifa Stars, Emmanuel Amuneke raia wa Nigeria.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini leo Ijumaa, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alikiri Amuneke kudai stahiki zake lakini FIFA haijawataarifu chochote kuhusu madai hayo.
"Mwalimu anatudai sehemu ndogo ya fedha za kusaini mkataba na bonasi baada ya kuiongoza kufuzu Fainali za Afcon.
"Kuhusu taarifa ya kutushitaki FIFA, binafsi kama suala hilo lingekuwepo, TFF ingeandikiwa barua kujulishwa lakini hadi sasa tunapozungumza FIFA hawajatuambia chochote juu ya jambo hilo.
"Kikubwa TFF kama taasisi tumejielekeza katika usimamizi mzuri wa masuala ya fedha, pia kuhakikisha hatuna madeni ndio maana tumelipa asilimia kubwa ya watu wanaotudai kwani lengo letu ni kufanya tuwe taasisi isiyodaiwa," alisema Kidao.
Kidao alisema Amuneke ambaye mkataba wake na TFF ulivunjwa Julai mwaka huu, alilipwa fedha za kuvunja mkataba huo na kwa sasa anadai kiasi kidogo cha fedha

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list