We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, September 11, 2019

Tamisemi yakiri uhaba walimu wa sayansi, yaomba kuajiri 15,000


Katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi 2018/19 Serikali ya Tanzania imeajiri watumishi 7,515 katika shule za sekondari nchini humo.

Kati ya watumishi hao, walimu walikuwa 7,218, fundi sanifu maabara 297 huku tatizo bado jambo ambalo limewafanya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuomba kibali cha kuajiri walimu 15,000.
Akijibu swali bungeni leo Jumatano Septemba 11, 2019, Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara ameliambia Bunge la Tanzania kuwa kati ya walimu walioajiriwa, 29 walikuwa wenye mahitaji maalumu, 50 elimu maalumu wakati masomo ya sayansi na hisabati walikuwa 7,089 ambapo Lugha (literature in English) wamepangwa 100.
Naibu Waziri alikuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Anna Lupembe ambaye amehoji ni lini Serikali itapeleka walimu wa sayansi katika mko wa Katavi.
Waitara amesema katika kipindi hicho Mkoa wa Katavi ulipangiwa watumishi 121 katika shule za sekondari ambapo walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ni 115 na fundi sanifu walikuwa sita.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list