We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, September 12, 2019

Mwinyi Zahera ameahidi kutoa dola 1000 kama Molinga hatofunga magoli 15 au 20

Kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema atatoa dola elfu moja (USD 1000)  kwa mwandishi wa habari endapo mchezaji wa Yanga raia wa Congo David Molinga asipofikisha magoli 20 au 15 msimu huu, kauli hiyo imekuja mapema leo wakati Yanga ikijiandaa na mchezo wa CAF Champions League dhidi ya Zesco United ya Zambia.
Kauli ya Zahera imekuja baada ya wengi kuonesha kutokuwa na amani na uwezo wa David Molinga licha ya yeye kuonesha kumuamini mchezaji huyo, Zahera anaamini hadi msimu unamalizika basi Molinga atakuwa kafunga magoli 15 hadi 20 na ikitokea hajafanya hivyo basi atatoa dola 1000.
Zahera anamwamini sana Molinga na kusema ni bora kuliko Makambo aliyeondoka Yanga na kujiunga na club ya AS Horoya, Molinga ametoka Congo akiwa amefunga magoli 15 akiwa katika Ligi yenye timu kubwa Afrika kama Tp mazembe, AS Vita na DC Motemapembe.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list