We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, September 13, 2019

Mtolea aeleza ushiriki wake, kwenye sakata la Meya

Mbunnge wa Temeke, Abdallah Mtolea, amesema yeye ni miongoni mwa wajumbe ambao wamesaini hoja ya kutokuwa na imani ya Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita, ambaye mwenyewe anatarajiwa kuwasilisha utetezi leo kwa Mkurugenzi.

Mbunge Mtolea amesema kuwa, "mimi niko Dodoma kwenye vikao vya Bunge kwa hiyo siwezi kulisema kwa sasa ila kila jambo linaloendelea na mimi nimeshiriki na ninaliunga mkono, kwa sababu mimi ni mmoja wa Wajumbe wa Baraza la Jiji na kila kinachoendelea mimi nipo."
"Kuhusu kuzungumzia kiundani kwa sasa siwezi kwa sababu nimeondoka wiki 2 zilizopita, ila kila jambo linaloendelea na mimi nipo ndani yake kwa sababu ni mjumbe wa Baraza hilo kupitia CCM," amesema Mtolea
Mapema jana akizungumzia tukio hilo, Meya wa Temeke Abdallah Chaulembo, alisema ni kweli wamefikisha malalamiko hayo na wanatarajia leo Septemba 13, 2019 kupokea majibu ya Meya Mwita.
Juhudi za kumpata Meya Isaya Mwita kwaajili ya ufafanuzi kwa upande wake bado zinaendelea.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list