“Nimeshiriki mazishi (ya Martha) familia yake isingeweza kunizuia kwa sababu inafahamu nini kinaendelea kati yangu na yeye. Kitendo cha kunikana si kipya na nilitarajia watafanya hivyo kwa sababu walishanikana siku nyingi,” amesema Mbosso leo Jumamosi Septemba 14, 2019 wakati akizungumza na Mwananchi.
Boss, Martha, msanii wa vichekesho wa kundi la Cheka Tu alifariki dunia Alhamisi Septemba 12, 2019 na kuzikwa jana Ijumaa jijini Dar es Salaam.
Amesema licha ya kumpinga tangu Martha akiwa hai, imani yake ni kuona siku moja familia ya mzazi mwenzie huyo ikiketi naye kujadili kuhusu mtoto aliyezaa na msanii huyo.
Amesema lengo lake si kumdai mtoto bali kueleza siri yake na Martha kuhusu kutoweka wazi suala la mahusiano yao, mtoto.
“Chochote nitakachofanya sasa nitaonekana ninafanya fujo, ndio maana nimeacha ili Martha niliyekuwa ninampenda sana apumzike kwa amani.”
“Hakuna mzazi anayemchukia mwanaye, ninajua ipo siku familia ya Martha itanipa mtoto wangu Ibrahim ambaye wao wanamuita Joseph,” amesema Mbosso.
Ameongeza, “Nilikuwa naletewa mara kwenye gari, siku nyingine nyumbani kwa Martha na wakati mwingine kwa rafiki zake. Anajua kuwa mimi ni baba yake nina imani siku moja tutakuwa pamoja akiniita baba na mimi nikimuita mwanangu.”

No comments:
Post a Comment