Simba imeendeleza umwamba wake kwenye ligi kuu ya Vodacom jioni hii baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-1 katika cmchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru
Meddie Kagere mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita, ameanza kuonyesha dalili mapema kuwa anakitaka kiatu cha dhahabu kwa msimu wa pili mfululizo baada ya leo kufunga bao lake la tatu msimu huu, akiifungia Simba bao la kuongoza kwenye dakika ya 16
Riphat Khamis aliisawazishia Mtibwa Sugar kwa mpira wa kona kwenye dakika ya 20
Hata hivyo Simba iliyokuwa imetawala mchezo huo kwa muda mwingi, ilijihakikishia ushindi katika dakika ya 68 kupitia kwa Miraji Athumani ambaye nae ameanza vyema msimu akifunga bao la pili
Ulikuwa ni mchezo ambao Simba ingeweza kuondoka na ushindi mnono zaidi kama ingetumia vyema nafasi nyingi walizotengeneza
Ushindi huo unawahakikishia mabingwa hao watetezi ushindi wa asilimia 100 msimu huu
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Lipuli Fc na utapigwa katika uwanja huo wa Uhuru
Mapema kabla ya mchezo huo Kagere alikabidhiwa zawadi yake baada ya kuibuka mchezaji bora wa VPL mwezi uliopita

No comments:
Post a Comment