Yanga imemaliza ziara yake mkoani Mwanza kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Toto African katika mchezo uliopigwa uwanja wa Nyamagana jioni ya leo
Mshambuliaji David Molinga ameendeleza moto wake wa mabao kanda ya ziwa akifunga mabao mawili kwenye dakika za 36 na 40
Bao la kwanza alimalizia kwa kichwa mpira uliotemwa na mlinda lango wa Toto baada ya kuokoa jaribio la Sadney.
Bao la pili akilifunga kwa ustadi mkubwa akimalizia kwa kichwa krosi ya Mrisho Ngasa
Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0
Kipindi cha pili kocha Mwinyi Zahera alibadili kikosi
Yanga ilihitaji dakika mbili tu kufunga bao la tatu kupitia kwa Abdulaziz Makame 'Bui' aliyepiga shuti kali akiwa nje ya 18
Mabingwa hao wa kihistoria sasa wanarejea jijini Dar es salaam kukamilisha maandalizi ya mwisho kabla ya kuikabili ZESCO United Jumamosi

No comments:
Post a Comment