Nahodha wa Simba John Bocco jana alianza mazoezi mepesi baada ya kuwa nje kwa wiki tatu akiuguza majeraha
Katika mazoezi ya jana yaliyofanyika uwanja wa Gymkhana, Bocco alipewa program maalum ya mazoezi yaliyosimamiwa kwa ukaribu na daktari wa timu
Bocco alikuwa nje tangu August 17 akiuguza majeraha ya goti aliyopata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc
Kurejea kwa Bocco ni habari njema kwa Simba katika kampeni yake ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo
Hata hivyo Bocco hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kitakachoikabili Mtibwa Sugar keshokutwa

No comments:
Post a Comment