We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, August 23, 2019

Zahera atamba kuboresha safu ya ushambuliaji Yanga


Kesho Jumamosi August 24 2019 Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa wa Botswana kuumana na Township Rollers kwenye mchezo wa marudiano michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa tisa Alasiri kwa saa za Botswana ambapo huku Tanzania itakuwa saa kumi
Kitu pekee ambacho Yanga inapaswa kufanya kesho ni kufunga angalau mabao mawili ili kujihakikishia nafasi ya kutinga raundi ya kwanza
Kama Yanga itafunga mabao mawili, Rollers watalazimika kufunga matatu ili waweze kufuzu
Lakini pia Yanga inahitaji ushindi wa aina yoyote ili iweze kusonga mbele
Kocha Mwinyi Zahera anafahamu mahitaji ya mchezo huo, jambo kubwa alilofanya kwa kikosi chake ni kuhakikisha kinafunga mabao mengi
Mcongomani huyo amesema kwa wiki nzima amekuwa akiwapa wachezaji wake mazoezi ya kuzifumania nyavu
"Tumefanya kazi kubwa sana kuhakikisha tunakuwa na matumizi mazuri ya mashambulizi tunayotengeneza," amesema Zahera
"Tumefanya mazoezi ya namna gani tunapaswa kwenda kushambulia na kujilinda vyema pale tunapokuwa hatuna mpira"
"Nafasi ya kufanya vizuri hapa Botswana tunayo, tumejipanga kupata ushindi"

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list