Kikosi cha Yanga tayari kiko Botswana kikiendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Mabingwa hao wa kihistoria walifanya mazoezi yao ya kwanza nchini humo jana baada ya kutua kimya kimya juzi jioni ikitokea Afrika Kusini
Kocha Mwinyi Zahera ametaka kikosi chake kiwasili Botswana mapema ili apate muda wa kutosha wa kufanya maandalizi ya mwisho pamoja na kuzoea hali ya hewa nchini humo ambapo kwa sasa ni baridi kali
Yanga inahitaji kuibuka na ushindi Jumamosi, hata matokeo ya sare ya kuanzia mabao 2-2 yataivusha Yanga hatua inayofuata
Mchezo huo utakaopigwa Jumamosi saa tisa Alasiri kwa saa za Botswana, utaamua timu itakayovuka raundi ya kwanza ambayo huenda ikachuana na ZESCO United katika hatua hiyo
ZESCO ilipata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Green Mamba uliopigwa huko eSwatini

No comments:
Post a Comment