Baada ya ushindi wa leo, Yanga imebakisha michezo miwili tu kujihakikisha kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Katika raundi ya kwanza Yanga itachuana na ZESCO United inayonolewa na George Lwandamina kocha wa zamani wa mabingwa hao wa kihistoria
Aidha kiungo Thabani Kamusoko anayecheza timu hiyo atakuwa na nafasi ya kukutana na waajiri wake wa zamani
Lakini habari njema zaidi kwa Yanga ni kuwa hata ikitolewa kwenye hatua hiyo, itashushwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho
Kwenye raundi ya kwanza mchezo wa kwanza utapigwa Zambia na marudiano kupigwa jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment