Wanyama mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na mwaka 2016 akitokea Southampton kwa ada ya Pauni 11 milioni na ametua katika klabu hiyo ya Ubelgiji kwa ada inayotajwa kuwa Pauni 9 milioni.
Club Bruges mapema mwezi huu ililippa pauni 6.4 milioni kwa kipa wa zamani wa Liverpool, Simon Mignolet kuonyesha inazidi kujiimarisha ili kuchuana na watetezi wa Jupiler, Genk anayoichezea Samatta ambaye walitambiana hivi karibuni katika Afcon 2019 nchini Misri, timu hizo zilipokuwa kundi moja sambamba na Algeria na Senegal.
Wanyama hakuwa na jinsi kuachwa na Spurs hasa baada ya kurejea kikosini kwa Harry Winks alityekuwa majeruhi tangu msimu uliopita, pia alikabiliwa na ushindano wa namba dhidi ya kiungo mpya aliyesajiliwa kwa dau la pauni 53.8 milioni Tanguy Ndombele.
Dau hilo ni rekodi kwa klabu hiyo ilifika fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita na kupoteza mbele ya Liverpool.
Katika msimu uliopita Wanyama alicheza mechi 13 tu kutokana na ushindani wa namba sambamba na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Tayari mchezaji huyo yupo Ubelgiji na taarifa zainasema amefanyiwa vipimo tayari kuanza kulianzisha nchini humo ambapo Samatta amekuwa gumzo kwa kuibeba Genk msimu uliopita na kuipeleka kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu ambapo Club Bruges nao wamo ikitanguliza mguu moja kwa kuifunga LASK Linz ya Austria kwa 1-0 nyumbani.
No comments:
Post a Comment