We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, August 20, 2019

Waliokula fedha Bil 3.4 wakabidhiwa TAKUKURU

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amekabidhi ripoti ya mkaguzi wa ndani wa hesabu za serikali kwa kamanda wa TAKUKURU wa wilaya ya Ukerewe, kufuatia ripoti hiyo kubainisha upotevu wa fedha za serikali zaidi ya shilingi bilioni 3.4.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo katika kikao maalumu cha baraza la madiwani cha kujadili hoja za mkaguzi wa ndani wa hesabu za serikali wilayani hapo na kumwagiza kamanda wa takukuru wilayani hapo kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa kwa wote watakaohusika na ubadhirifu huo wa fedha.
''Haiwezekani mkawa watu wa hivi, kwamba mna Bil 3.4 za kula tu, kamanda wa TAKUKURU wa wilaya nenda kashughulikie hili na asionewe mtu'', amesema Mkuu wa mkoa.
Aidha amebainisha kuwa fedha hizo zilikuwa zikitakiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka 2017/2018 katika wilaya ya Ukerewe.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list