We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, August 19, 2019

Rais wa Zaman wa Sudan Omar al-Bashir Mahakamani Tena Leo....Amekiri Kupokea Rushwa ya dola milioni 90 na Saudi Arabia

Upande wa mashitaka katika kesi ya ufisadi inayomkabili rais wa zamani wa Sudan, Omar al-Bashir, umeiambia mahakama mjini Khartoum leo kuwa kiongozi huyo amekiri kupokea dolamilioni 90 taslimu kutoka kwa Ufalme wa Saudia Arabia.

Brigadia Ahmed Ali alisema Bashir alimuambia kuwa malipo ya mwisho yaliwasilishwa kwake na baadhi ya wajumbe wa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia, Mohammed bin Salman. 

Afisa huyo wa upelelezi aliiambia mahakama kuwa walikuta kiasi cha euro milioni saba pamoja na kiwango kidogo cha dola za Kimarekani na paundi za Sudan kwenye makaazi ya Bashir, ambaye alisema zilikuwa sehemu ya kitita chadola milioni 25 ambazo Bin Salman alimpa kwa matumizi yaliyo nje ya bajeti. 

Bashir alisema alikuwa amepokea malipo mara mbili ya dola milioni 35 na milioni 30 kutoka kwa Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia aliyefariki dunia mwaka 2015. 

Bashir ambaye aliitawala Sudan kwa miaka 30, alifikishwa mahakamani leo akisindikizwa na msafara mkubwa wa kijeshi.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list