Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, leo Agosti 24, amezindua hotel ya Madinat El Bahr mjini Unguja, itakayoweza kuchangia asilimia 27 ya pato la Taifa na asilimia 80 ya fedha za kigeni.
Akizungumza katika hotuba yake Dkt Shein amesema, idadi ya watalii wa kimataifa waliofika Zanzibar tangu mwaka 2008 hadi mwaka huu imekuwa ikiongezeka kwa kiwango kizuri, ambapo hadi Desemba mwaka 2018 idadi ya watalii waliotambelea visiwani humo walikuwa 520,809.
''Kwa mujibu wa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania, sekta ya utalii inachangia asilimia 80 ya fedha za kigeni, zinazoingia Zanzibar na kwa miaka kumi iliyopita, utalii umechangia kiasi kikubwa katika upatikanaji wa ajira'' amesema Dkt Shein.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali pamoja na wawekezaji mbalimbali katika sekta ya utalii.
No comments:
Post a Comment